← SBS Swahili - SBS Swahili
Taarifa ya Habari: Wito watolewa kutokomeza unyanyasaji wa nyumbani nchini Australia artwork

Taarifa ya Habari: Wito watolewa kutokomeza unyanyasaji wa nyumbani nchini Australia

SBS Swahili - SBS Swahili
05:39
Play episode

Show notes

Ripoti mpya kati ya vizazi imetolewa leo, ikionyesha athari za bajeti ya serikali na mitazamo ya uchumi katika miongo minne ijayo. Naibu Kamishna wa Polisi wa New South Wales Peter McKenna anasema matukio manne tofauti yanayodaiwa kuwa ya unyanyasaji wa nyumbani mwishoni mwa wiki iliyopita yanaonyesha uzito wa janga hilo nchini Australia. Katika tukio lililo ripotiwa katika eneo la Blue Mountains, mvulana wa miaka mitano alikufa, na ndugu zake wawili na mama yake mwenye umri wa miaka 42 walijeruhiwa vibaya baada ya kupatikana na majeraha ya kudungwa visu ndani ya gari katika eneo la Valley Heights. Kenya imetetea makampuni ya ndani yanayoagiza mafuta yaliosafishwa chini ya makubaliano ya serikali kwa serikali, siku chache baada Kampala kudai kuwa mpango huo ulikuwa umetekwa na madalali hali iliyopelekea kupanda kwa bei ya mafuta nchini Uganda. Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa nishati nchini Kenya, Opiyo Wandayi, kampuni kubwa tatu za mafuta katika nchi za Ghuba zinazouza mafuta yake nchini Kenya, zilichagua kampuni za ndani katika mpango huo na kwamba ikiwa serikali ingesisitiza kuchagua makampuni hayo basi mpango huo ungekufa. Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.

More from this show

More
  1. Yaliyojiri Afrika:Rais wazamani wa DRC atuhumiwa kwa kujaribu kupindua serikali ya sasa

    Kwa zaidi ya miongo miwili, Joseph Kabila amekuwa mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa katika siasa za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

    06:59
  2. Taarifa ya Habari:Uchunguzi waendelea baada ya mbunge wa Shirikisho, Helen Haines, kugongwa na gari nje ya ofisi yake ya uwakilishi

    Polisi wa Victoria wanasema hakuna tishio lolote linaloendelea dhidi ya mtu mwingine au jamii kwa ujumla, kufuatia tukio ambapo Mbunge wa Shirikisho, Helen Haines, aligongwa na gar…

    15:31
  3. How laws change, and why it takes time | How Australia Works - Jinsi sheria hubadilika, na kwa nini huchukua muda| How Australia Works

    How do laws change in Australia? Through Rodney Croome’s campaigns for human rights and marriage equality, learn how personal stories, community action, courts and parliament can h…

    07:33
  4. Taarifa ya Habari:Serikali ya shirikisho yatupilia mbali wazo la kuongeza kodi ya bidhaa na huduma (GST)

    Taasisi ya Grattan inaitaka serikali kuongeza kiwango cha kodi ya bidhaa na huduma (GST) kutoka asilimia 10 hadi asilimia 15, ikiwa ni sehemu ya marekebisho makubwa ya bajeti.

    05:39
  5. Chairmodo "michuano hii inatupa fursa ya kusherehekea utamaduni wetu"

    Vijana wa jumuiya zawa Kenya kutoka majimbo na wilaya za Australia, walijumuika mjini Adelaide 3-4 Oktoba kwa michuano ya kombe la Kenya All Stars.

    12:33
  6. Makala Leo:Maana ya kuongezeka kwa dhiki ya kiuchumi nchini Australia kwako

    Dhiki ya kiuchumi nchini Australia inazidi kuongezeka. Uchambuzi mpya kutoka kwa Kamati ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Australia (CEDA) umebaini kuwa hali hiyo imerejea karibu na viwa…

    09:36
Now Playing
Taarifa ya Habari: Wito watolewa kutokomeza unyanyasaji wa nyumbani nchini Australia — SBS Swahili - SBS Swahili | Podcast | Josplay Music